Ngeli ni kundi la majina lenye sifa zinazofanana.
Ngeli ya A-WA
Majina katika ngeli hii huwa yanajumuisha majina ya viumbe vyenye uhai kama wanyama, wanadamu, wadudu, ndege, samaki na viumbe vingine vinavyoishi majini.
Mifano
Mwalimu ameingia darasani – Walimu wameingia darasani
Daktari amemtibu mgonjwa – Madaktari wamewatibu wagonjwa
Paka ameikunywa maziwa yote – Paka wameikunywa maziwa yote.
Kipepeo yule amekanyagwa na nani? – Vipepepeo wale wamekanyagwa na nani?
Kuku ametaga yai chumbani mwangu. – Kuku wametaga mayai chumbani mwetu.
Ngeli ya LI-YA
Maneno katika kikundi hiki huanza kwa silabi ma au me.
Mifano
Kabati lilikuwa na mende – Makabati yalikuwa na mende.
Jiwe lililorushwa liliniumiza – Mawe yaliyorushwa yalituumiza.
Dirisha lilifungwa na mwanafunzi – Madirisha yalifungwa na wanafunzi.
Yai lilivunjika lilipoangushwa chini – Mayai yalivunjika yalipoangushwa chini.
Ngeli ya U-I
Ngeli hii hujumuisha majina ya miti, mimea na baadhi ya viungo vya mwili. Nomino hizi huanza kwa herufi M, MW, MU. MI. Vitenzi vinavyotumika na majina ya ngeli hii huanza na U kwa umoja na I kwa wingi.
Mifano
Mti uliochomeka jana ndio huu. – Miti iliyochomeka jana ndio hii.
Mswaki wangu uko wapi? – Miswaki yetu iko wapi?
Mkono unauma.- Mikono inauma.
Muhogo umewekwa pilipili. – Mihogo imewekwa pilipili.
Mwavuli umeraruliwa na mtoto. – Miavuli imeraruliwa na watoto.
Ngeli ya KI-VI
Nomino katika ngeli ya KI-VI huhusisha maneno ambayo huanza kwa kiambishi ki au ch katika umoja na vi au vy katika wingi.
Mifano
Kitabu kimeraruliwa na mbwa. – Vitabu vimeraruliwa na mbwa
Kiatu kinanuka vibaya. – Viatu vinanuka vibaya
Kiti kilivunjika na kumuumiza. – Viti vilivunjika na kuwaumiza.
Chakula kilipikwa na nani? – Vyakula vilipikwa na nani?
Chuo kilifungwa baada ya simba kuingia humo. – Vyuo vilifungwa baada ya simba kuingia humo.
Chandarua kiliwekwa kabatini – Vyandarua viliwekwa kabatini.
Ngeli ya LI-LI
Giza limezidi. Giza limezidi.
Jua lilifunikwa na mawingu. Jua lilifunikwa na mawingu.
Jasho jingi lilimtoka. Jasho jingi liliwatoka.
Ngeli ya I-ZI
Saa yangu imeharibika -Saa zangu zimeharibika
Kalamu yangu imepotea darasani – Kalamu zangu zimepotea darasani
Rula yangu iko mezani – Rula zangu ziko mezani
Nyumba yangu ni kubwa – Nyumba zangu ni kubwa.
Chupa yangu imejaa maji – Chupa zangu zimejaa maji.
Ngeli ya I-I
Zoezi : Ngeli ya A-WA, KI-VI, I-ZI
Zoezi: Ngeli Za Kiswahili
Mvua ilinyesha usiku mzima. – Mvua ilinyesha usiku mzima
Huzuni ilimpata baada ya mtu huyo kufariki. – Huzuni iliwapata baada ya watu hao kufariki.
Asali hutengenezwa na nyuki. – Asali hutengenezwa na nyuki.
Hasira ilimshika alipoona mtoto huyo akichapwa. – Hasira iliwashika walipoona watoto hao wakichapwa
Ngeli ya YA-YA
Nomino katika ngeli hii huchukua kiambishi ‘ya’ kwa umoja na kwa wingi. Pia, nomino katika ngeli hii huanza na kiambishi ‘ma’ kwa umoja na kwa wingi.
Marashi ya mama yananukia vizuri. Marashi ya mama yananukia vizuri.
Maji yalimwagika sebuleni. Maji yalimwagika sebuleni.
Mafuta yameharibika. Mafuta yameharibika.
Utagundua ya kwamba, nomino hizi haziwezi hesabika.
Ngeli ya U-ZI
Nomino hizi huwa na ‘u’ katika umoja na ‘zi’ katika wingi. Baadhi ya nomino hizi huanza na u katika umoja (au w) na ny katika wingi.
Uso wako umeparara – Nyuso zenu zimeparara.
Uwanja huo ni mchafu – Nyanja hizo ni chafu.
Uzi wangu umepotea. Nyuzi zetu zimepotea.
Wembe ule ulimkata – Nyembe zile ziliwakata.
Wimbo huo umefanya ni lale – Nyimbo hizo zimefanya ni lale.
Ni muhimu kwa wanafunzi kuelewa ngeli ili wapate alama bora katika mtihani wa Kiswahili.
